Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool yaomba Mo Salah aachwe

Salah Return AXA Liverpool yaomba Mo Salah aachwe

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Liverpool imekiomba chama cha soka cha Misri kisimjumuishe Mohamed Salah kwenye kikosi kijacho cha timu ya taifa ili kumsaidia winga huyo apone kabisa majeraha yake. Staa huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa sasa yupo kwenye chumba cha wagonjwa akipatiwa matibabu ya maumivu ya paja, tatizo ambalo alilipata alipokuwa akiitumikia Misri kwenye Afcon 2023.

Mo Salah alirejea mapema Liverpool kwenda kupatiwa matibabu wakati michuano ya Afcon 2023 ikiwa inaendelea huko Ivory Coast na kulikuwa na matumaini kwamba angerejea tena kuitumikia timu yake, lakini Misri ilikomea hatua ya 16 Bora baada ya kutupwa nje kwa mikwaju ya penalti na DR Congo.

Mo Salah alirejea uwanjani kwenye mechi dhidi ya Brentford, Februari 17, ambapo alifunga na kuasisti akiwa ametokea benchi kwenye ushindi wa 4-1, lakini alitonesha misuli yake katika mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Gtech Community.

Tangu wakati huo Mo Salah hakucheza tena kwenye kikosi hicho cha Jurgen Klopp, akikosa mechi zote nne za michuano iliyocheza Liverpool, ikiwamo fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Chelsea.

Na hata mechi ijayo ya hatua ya 16 Bora ya Europa League dhidi ya Sparta Prague, nayo inaweza kuwa mapema sana kwa Mo Salah kurejea uwanjani, lakini kuna matumaini ya kuwamo kwenye kikosi cha Manchester City, wikiendi ijayo. Mwezi huu kutakuwa na mapumziko ya mechi za kimataifa, ambapo Misri itakipiga na New Zealand (Machi 22) na ama Croatia au Tunisia (Machi 25/26).

Chanzo: Mwanaspoti