Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool yampotezea Ollie Watkins

Ollie Watkins Ascd Ole Watkins

Wed, 12 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Habari ndo hiyo. Liverpool imeripotiwa kufuta dili zote sita za mastaa ambao ilipanga kuwasajili kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya, ikiwamo straika wa Aston Villan, Ollie Watkins.

Liverpool itakuwa chini ya kocha mpya Arne Slot, ambaye ametua huko Anfield kuchukua mikoba ya Mjerumani Jurgen Klopp.

Nje ya uwanja, Michael Edwards amekuwa akifanya kazi kubwa na kushirikiana na wengine kwenye dili za usajili, sambamba na Richard Hughes, ambaye atatua kwenye kikosi hicho kwenda kuwa mkurugenzi mpya wa michezo, ambao watafanya kazi kubwa ya kusajili mastaa wapya ili kuifanya Liverpool kuwa na nguvu ya kushindania mataji msimu ujao.

Lakini, taarifa za ndani zinadai kuna dili sita za mastaa ambao iliwataka, zote zimefutwa, ikianzia ya Watkins wa Aston Villa.

Dili nyingine iliyofutwa ni ya fowadi wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz, ambaye aliisaidia timu hiyo kubeba Bundesliga msimu uliopita bila kupoteza mechi.

Slot alimtaka pia staa wake wa zamani Yankuba Minteh, lakini dili hilo halitafanyika kama ilivyo kwa mkali wa Atalanta, Ederson, ambaye aliisaidia timu hiyo kushinda ubingwa wa Europa League. Pauni 40 milioni anazouzwa kiungo huyo ndicho kitu kilichowafanya Liverpool isitishe mpango wa kunasa saini yake.

Kutokana na kuachana na beki Joel Matip, staa wa Sporting Lisbon, Goncalo Inacio alihusishwa na Liverpool, lakini sasa mchezaji huyo hakuna namna ambayo atakwenda kukipiga kwenye Ligi Kuu England akiwa na wababe hao wa Anfield, kutokana na kusitishwa kwa mpango wa kumsajili.

Bei kubwa anayouzwa Alan Varela, anayekipiga kikosini FC Porto, ambaye pia alikuwapo kwenye rada za Liverpool, naye hatasajiliwa na miamba hiyo ya Anfield, ikijaribu kufanya matumizi mazuri ya mkwanja wao kwenye usajili wa dirisha hili ili kwenda sawa na kanuni za mapato na matumizi ya Ligi Kuu England kama zinavyoelekeza kwa timu zote zinazoshiriki ligi hiyo yenye ushindani mkali.

Chanzo: Mwanaspoti