Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool yakamilisha makundi kwa ushindi, Salah akiweka rekodi

Liver Winner Vs Milan Wachezaji wa Liver wakishangilia goli la Salah dhidi ya Milan

Wed, 8 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majogoo wa Jiji Liverpool wamekamilisha hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa barani Ulaya usiku wa jana kwa kuichapa AC Milan ndani ya dimba la San Siro magoli 2-1.

Liverpool ambao tayari walishakata tiketi ya kufuzu kwa hatua ya 16 bora, walifanya mabadiliko makubwa katika kikosi chao kilichoanza jana, kwa kupumzisha idadi kubwa ya wachezaji wanaoanza mara kwa mara.

AC Milan ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli katika mchezo huo likiwekwa wavuni na mlinzi F. Tomor dakika ya 29, kabla ya Salah kuisawazishia Liver dakika ya 36 kisha D. Origi akaiandikia liver bao la pili na la ushindi dakika ya 55.

Goli alilofunga Mohammed Salah ni la Saba katika hatua ya makundi na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Liverpool kufunga idadi hiyo ya magoli katika hatua ya Makundi.

Kwa matokeo hayo Liver imemaliza kinara wa kundi B kwa kujikusanyia alama 18 baada ya michezo 6, Atletico nafasi ya pili wakiwa na alama saba, Porto nafasi ya tatu wakiwa na alama 5 huku Milan akiburuza mkia kwa alama zake 4.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live