Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool yajitosa mazima kwa Ollie Watkins

Ollie Watkins Ascd Ollie Watkins.

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Liverpool imeendelea kupambana kwa ajili ya kumsajili straika wa Aston Villa, Ollie Watkins katika dirisha hili kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ushambuliaji ambalo msimu ujao huenda likamkosa Mohamed Salah anayetajwa kuwa kwenye mpango wa kataka kujiunga na Al Ittihad ya Saudi Arabia.

Mabosi wa Liverpool wamevutiwa sana na kuwango cha Watkins alichoonyesha msimu uliopita na alifunga mabao 19.

Kusajiliwa kwa Watkins pia kunatajwa kusababishwa na kitendo cha Barcelona kutaka kumsajili Darwin Nunez.

Kocha mpya wa majogoo hawa wa Jiji la Liverpool, Arne Slot anataka kujenga upya timu na amewaambia wachezaji ambao hawahitaji kubaki kuwa milango ipo wazi.

Hata hivyo, inaonekana kuwa itakuwa ngumu kwa Liverpool kumpata staa huyu kwa bei rahisi kwani ndio mchezaji tegemeo katika safu ya ushambuliaji ya Villa na bado ana mkataba wa zaidi ya misimu mitatu mbele.

Kingine kinatajwa itakuwa ngumu kwa sababu Villa pia itashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao na hawataki kuuza wachezaji wao muhimu ili wawasaidie kwenye michuano hiyo mikubwa inayoshiriki kwa mara ya kwanza.

Arsenal inaangalia uwezekano wa kumsajili winga wa Girona raia wa Ukraine, Viktor Tsygankov, 26, katika dirisha hili la majira ya kiangazi na watakumbana na upinzani wa kutosha kutoka kwa AC Milan ambayo ilianza kumfuatilia tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Viktor ni mmoja kati ya mastaa waliofanya vizuri msimu uliomalizika na huenda akaondoka kutokana na kutakiwa na miamba mingi Ulaya.

Chelsea ina uhakika wa asilimia nyingi juu ya kuipata huduma ya mshambuliaji wa RB Leipzig, Benjamin Sekso anayewindwa pia na Arsenal zikihitaji kumsajili dirisha hili. Sesko (21), ameziingiza timu nyingi kwenye vita kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu. Chelsea inataka kujenga upya safu yao ya ushambuliaji na mbali ya Sesko pia inahusishwa na Napoli.

Manchester United imewaweka kwenye rada mabeki watatu ambao mmoja wao ina matumaini ya kumsajili dirisha hili. katika orodha hiyo ya mabeki watatu mmoja wao ni Jarrad Branthwaite, 21, kutoka Everton ambaye ndio anapewa kipaumbele zaidi ingawa pia yupo beki wa Juventus na Brazi lGleison Bremer, 27, pamoja na beki wa Nice na Ufaransa Jean-Clair Todibo, 24.

West Ham inajaribu kuipiku Bayer Leverkusen kwenye mchakato wa kuiwania saini ya kiungo wa Girona, Mhispania Aleix Gargia, 26, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Garcia ni mmoja wa mastaa tegemeo Girona akionyesha kiwango bora msimu uliopita kiasi cha Leverkusen kuanza mazungumzo ya kumsajili. Kuingia kwa West Ham kwenye dili kunaisababishia ugumu Leverkusen.

MABOSI wa West Ham wanatarajia kutuma wawakilishi wao kwenda Ureno kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Vitoria Guimaraes ili kumsajili winga wa timu hiyo, Jota Silva katika dirisha hili. Jota mwenye umri wa miaka 24, amekuwa kwenye rada za timu nyingi ikiwemo Crystal Palace kutokana na kiwango alichoonyesha msimu uliomalizika.

BEKI kisiki wa Fulham, Tosin Adarabioyo, 26, ameshafanya vipimo vya afya kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Chelsea dirisha hili. Taarifa zinaeleza kila kitu kipo sawa na kilichokuwa kinasubiriwa ni vipimo vya afya na kusaini mkataba. Mkataba wa Adarabioyo na Fulham unatarajiwa kumalizika mwisho wa mwezi huu.

Tottenham ipo tayari kumwachia beki wao. Djed Spence, 23, kujiunga na Genoa kwa mkataba wa kudumu dirisha hili ikiwa timu hiyo itawapa ofa itakayowashawishi. Spence alionyesha kiwango bora alipokuwa akicheza kwa mkopo Genoa kwa msimu uliopita hali iliyolivutia benchi la ufundi na kupendekeza abaki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live