Klabu ya Chelsea ilikuwa mstari wa mbele katika kinyang’airo cha kuipata saini ya beki wa kati wa Barcelona Ronald Araujo sasa taarifa za hivi karibuni zinadai kwamba Liverpool wapo karibu kumnasa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay.
Chelsea itawabidi waongeze dau ili kumvutia mchezaji na klabu ili kuipata saini ya mchezaji huyo wa miaka 22 kwa kuwa walinzi wao Antonio Rudiger na Andrea Christensen mikataba yao inaelekea kuisha huko Darajani.
El Nacional inaeleza kuwa Araujo analengwa sana na Liverpool, ambao wana Joe Gomez na Joel Matip waliorejea dimbani baada ya kusumbuliwa na majeraha kama chaguo la beki wa kati pamoja na Van Dijk.
The Reds pia walimwagia pesa kibao kwa Ibrahima Konate katika dirisha la usajili wa majira ya joto la 2021, lakini Mfaransa huyo amecheza kidogo hadi sasa, huku Matip akiwa chaguo bora zaidi pamoja na Van Dijk.
Lakini, kukiwa na majeruhi bado wasiwasi linapokuja suala la Matip, Araujo anaweza kuwa chaguo muhimu kwa kupokezana na mbadala kuongoza safu ya ulinzi ya Liverpool katika siku zijazo.
Barcelona bado wanapambana na changamoto za kiuchumi hivyo watalazamika kuuza wachezaji ili kuendelea kuboresha mfuko wako.