Liverpool imeichapa bao 1-0 Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa Leo Jumamosi dimba la St James, ushindi wa Liverpool unaendeleza kutoa presha dhidi ya timu kinara wa Ligi hiyo Manchester City.
Mechi nne zimebakia baina ya timu hizo lakini tofauti ya pointi moja imeendelea kuleta ushindani mkali na kwa namna ambavyo mambo yanaenda si ajabu yeyote atakayeangusha hata alama mbili kwa maana ya sare atakuwa “ametupa taulo”.
Kabla ya mechi hiyo, Newcastle United walikuwa hawajapoteza katika mechi 4 za nyumbani St James lakini bao la kipindi cha kwanza la kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Guinea Naby Keita limewapa utofauti baina ya timu hizo mbili.
Baada ya mchezo huo ambao kocha Jurgen Klopp alikuwa amefanya mabadiliko ya wachezaji watano akiwemo staa Mohamed Salah atakuwa anaelekea Hispania kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Uefa na Villarreal, ambao wanaenda wakiwa kifua mbele kwa ushindi wa bao 2-0 walioupata Anfield.