Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool yaichapa Ajax Ligi ya Mabingwa

Matip Scores Winner For Liverpool Vs Ajax 1200x630 Matip alifunga bao la ushindi la Liverpool

Wed, 14 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majogoo wa Jiji, Timu ya Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ajax katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Uwanja wa Anfield.

Liverpool ambao wana mwendo wa kusua sua tangu kuanza kwa msimu huu ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Mohamed Salah dakika ya 17, kabla ya Mohammed Kudus kuisawazishia Ajax dakika ya 27 na kufanya matokeo kuwa 1-1.

Wakati mchezo ukielekea ukingoni, mlinzi Joel Matip akawahakikishia Liver kuondoka na alama tatu kwa goli la dakika ya 89 lililowapa ushindi Liverpool.

Mchezo huo kati ya Liver na Ajax ulikuwa ni wa hatua ya makundi, kundi A.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live