Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool yafufua upya mbio za Ubingwa EPL

Palace Vs Liver Wachezaji wa Liverpool wakimpongeza Fabinho baada ya kupachika bao la tatu

Mon, 24 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bila ya uwepo wa Nyota wake watatu wanaofanya vyema ndani ya kikosi hicho, Mane, Salah na Keita majogoo wa Jiji, Timu ya Liverpool wamechukua alama tatu katika mechi ngumu dhidi ya Crystal Palace katika dimba la

Ushindi huo wa Liverpool unaongeza chachu ndani ya kikosi hicho baada ya siku ya Jumamosi kinara wa EPL Man City kutoa sare na Southampton na hivyo kufanya mbio za Ubingwa kuonekana zimefufuka upya baina ya liver na City.

Mabao ya Liverpool yamefungwa na mlinzi wa kati raia wa Uholanzi Virgil van dijk akimalizia mpira wa kona wa beki wa kushoto Andy Robertson, Alex Oxlade-Chamberlain kabla ya presha ya kipindi cha pili ya Palace na kupata bao la kufutia machozi la Odsonne Eduard bao la tatu kwa Liverpool limefungwa na Fabinho kwa mkwaju wa penati baada ya Jota kuangushwa eneo la hatari.

Ushindi huo wa Liverpool unawafanya kufikisha alama 48 huku wakiwa nyuma kwa alama tisa nyuma ya Vinara Man City, huku Liverpool wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live