Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool yaendeleza ubabe EPL, Waichapa Burnley

Nunez Headrer Liverpool yaendeleza ubabe EPL, Waichapa Burnley

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Liverpool imepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Burnley na kuendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England, Premier.

Awali Manchester City ilitishia nafasi ya Liverpool kileleni na kukaa hapo kwa dakika chache baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton.

Ushindi wa Liverpool, umeifanya ifikishe pointi 54 ikiwa ni pointi moja mbele ya Man City yenye 53, lakini ina faida ya mchezo mmoja mkononi

Mabao ya Liverpool kwenye mchezo huu yalifungwa na Diago Jota dakika ya 30, Luis Diaz dakika ya 52 na Darwin Núñez 79, huku bao pekee la Burnley likifungwa na Dara O'shea dakika 45.

Mechi nyingine imeshuhudia Tottenham Hotspur ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Brighton.

Mechi nyingine kali za ligi hiyo zitaendelea kesho wakati Man United itakapovaana na Aston Villa na Arsenal dhidi ya wababe West Ham

Chanzo: www.tanzaniaweb.live