Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool watonywa njia ya kurudisha makali yao

Danny Murphy Mkongwe wa Liverpool, Danny Murphy

Sat, 25 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa Liverpool, Danny Murphy ameuomba uongozi wa Liverpool ifanye usajili wa nguvu kuboresha maeneo ya kikosi msimu mpya utakapomalizika.

Kauli hiyo aliisema baada ya Liverpool kudhalilishwa na kupokea kichapo cha mabao 5-2 dhidi ya Real Madrid kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya 16 bora ya Ligi Mabingwa Ulaya uliyochezwa Jumanne, usiku uwanja wa Anfield.

Hiko ni kipigo cha kwanza kizito kwa Liverpool kutokea uwanja wa Anfield kwenye michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya katika historia ya klabu hiyo, lakini mkongwe huyo anaamini Jurgen Klopp ana kazi ya kujenga kikosi kipya msimu ujao.

Liverpool iliondolewa kwenye mashindano ya ligi na ipo nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu England licha ya kushinda mechi zao mbili zilizopita.

Sasa Liverpool ipo mguu nje kwenye michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya ina kazi kubwa ya kupindua matokeo dhidi ya Madrid katika mechi ya marudiano itakayochezwa Santiago Bernabeu wiki ijayo.

Wachezaji kama Fabinho na Joel Matip ni miongoni mwa wachezaji ambao mkongwe huyo anaamini hawastahili kuwepo kikosini msimu ujao.

"Nafikiri muda wa kuboresha kikosi umefika, wachezaji watano au sita wanatakiwa kuuzwa, Klopp anafahamu hilo, Klopp atapata nafasi ya kufanya mabadiliko katika kikosi chake, je itakuwa rahisi kuwaachia wachezaji? mashabiki wapo pamoja na mimi, tusubiri kuona, nadhani usajili utakuwa zaidi ya wachezaji watano au sita dirisha la usajili la kiangazi," alisema mkongwe huyo

Murphy anaamini wachezaji kama Naby Keita, Alex Oxlade-Chamberlain, James Milner maisha yao ndani ya viunga vya Anfield yanaelekea ukingoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live