Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool watinga nusu Fainali Carabao Cup

IMG 8012.jpeg Liverpool watinga nusu Fainali Carabao Cup

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Liverpool FC jana wametinga Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England kwa ushindi wa kishindo wa mabao 5-1 dhidi ya West Ham United Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.

Mabao ya Liverpool yamefungwa na Dominik Szoboszlai dakika ya 28, Curtis Jones dakika ya 56 na 84, Cody Gakpo dakika ya 71 na Mohamed Salah dakika ya 82, huku la West Ham likifungwa na Jarrod Bowen dakika ya 77.

Sasa Liverpool itakutana na Fulham iliyoitoa Everton juzi kwa penalti 7-6 baada ya sare ya 1-1, wakati Nusu nyingine ni katí ya Chelsea na Middlesbrough.

Chelsea iliitoa Newcastle United kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 1-1 na Middlesbrough iliitandika Port Vale 3-0 katika mechi za juzi za Robó Fainali ya michuano hiyo inayojulikana kama Carabao Cup.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live