Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool watinga Fainali ya UEFA, waichapa Villarreal

Liver Merseyside Liverpool wakishangilia usiku wa jana

Wed, 4 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Liverpool wamelazimika kutokea nyuma na kuibuka na ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Villarreal katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya nusu fainali mkondo wa pili uliofanyika nchini Hispania.

Wakiingia kwenye mechi hiyo wakiwa na faida ya goli 2-0 kupitia magoli ya mchezo wa raundi ya kwanza, Liverpool walibanwa vilivyo na kuifanya Villarreal kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza bao 2-0 na hivyo kufanya matokeo yawe 2-2 goli mbili za Liverpool Nyumbani na goli mbili za Villarreal mchezo wa Leo.

Hata hivyo, kipindi cha pili majogoo wa jiji la Merseyside walionyesha utofauti hasa kwa kuingia Luis Diaz akitoka Diogo Jota kulipeleka ndani ya muda mfupi kufunga magoli matatu, akitangulia kufunga Fabinho kabla ya Diaz mwenyewe kuvunja mtego wa kuotea na kufunga bao kupitia pasi ya Trent Alexander Arnold kisha Sadio Mane akaingia kambani bao la tatu.

Ambapo sasa Liverpool wanafuzu kucheza fainali ya Uefa kwa jumla ya goli 5-2.

Mabao ya Villarreal yamefungwa na Boulaye Dia dakika ya tatu ya mchezo kabla ya kiungo mkabaji wa zamani wa Arsenal Francis Coquelin kufunga bao la pili akitumia krosi dongo ya Capoue.

Nyambizi wa Kijani wamemaliza pungufu kufuatia Capoue kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya mchezo usiokuwa wa kiungwana kwa Curtis Jones.

Hakuna timu yoyote ambayo imewahi kushinda mataji manne nchini England kwa maana ya Ligi ya Mabingwa, Kombe la FA, Carabao na Ligi Kuu Liverpool wako kwenye mbio za kuwania mataji hayo manne na itakuwa timu ya kwanza kufanya hivyo kama watafanikiwa.

Mchezo wa fainali ya Uefa utapigwa Paris nchini Ufaransa Mei 25, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live