Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool wasitisha Mazoezi Kuelekea Mchezo dhidi ya Arsenal

Axa Liverpool yasitisha mazoezi kisa visa vya Corona

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Liverpool jioni ya jana imesitisha mazoezi ambayo yalipangwa kufanyika kutokana na kuongezeka kwa visa vya Uviko-19 kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Carabao Cup

Mchezo wa Carabao Cup wa nusu fainali kati ya Liverpool na Arsenal upo kwenye hatari ya kuweza kuahirishwa kutokana kuongezeka visa vya Uviko-19 katika upande wa klabu ya Liverpool.

Inaeleweka kuwa majogoo wa Anfield walikuwa waanze mazoezi jana jioni, lakini yamehairishwa huku mchezo wao ukiwa umepangwa kuchezwa siku ya tarehe ya 6/1/2022 alhamisi, mpaka muda huu hakuna taarifa yeyote ya kuahirishwa kwa mchezo huo japo klabu ya Liverpool wapo kwenye mazungumzo na EFL.

Ikiwa timu zote zitakuwa na wachezaji 14 wakiwemo makipa wawili, basi mchezo utaendelea kama kawaida, awali Majogoo iliwakosa wachezaji wake tisa wa kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Chelsea, huku pia wakiwapoteza wchezaji wake mahiri Mohamed Salah, Sadio Mane na Naby Keita ambao wamerudi Afrika kucheza AFCON.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live