Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool wapiga mtu bao 4 Uropa

IMG 6371.jpeg Wachezaji wa Liverpool wakishangilia mabao yao

Fri, 1 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Liverpool wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya LASK ya Austria katika mchezo wa Kundi E UEFA Europa League usiku wa Alhamisi Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool, England.

Mabao ya Liverpool yamefungwa na Luis Diaz dakika ya 12, Cody Gakpo mawili, dakika ya 15 na 90 na ushei na Mohamed Salah dakika ya 51 kwa penalti.

Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 12 na kufuzu Hatua ya 16 Bora ya UEFA Europa League mbele ya Toulouse ya Ufaransa yenye pointi nane, Royal Union St-Gilloise ya Ubelgiji yenye pointi tano na LASK pointi tatu baada ya mechi tano kwa wote kuelekea mechi za mwisho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live