Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool wamrudisha tena Jurgen Klopp

Lfc Foundation Klopp Ambassador Cover 090724 Jurgen Klopp

Mon, 15 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jurgen Klopp amerejea tena Liverpool ikiwa ni miezi kadhaa tangu atangaze kuachana na timu hiyo na sasa amepewa cheo cha kuwa balozi wa heshima wa taasisi ya Liverpool.

Klopp ambaye aliachana na Liverpool mwisho wa msimu uliopita ni miongoni mwa makocha waliopata mafanikio makubwa na timu hiyo akiiwezesha kushinda taji la Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu England na msimu wake wa mwisho aliisaidia kuchukua taji la Carabao.

Katika mchezo wa mwisho akiwa na Liverpool aliisaidia taasisi hiyo ambayo kazi yake ni kutoa misaada na kurudisha kwa jamii kukusanya jumla ya Pauni 40,000 ambayo ilitokana na mauzo ya vitu mbalimbali ambavyo aliweka saini yake.

Kocha huyu mwenye umri wa miaka 57, baada ya kuachana na Liverpool amekuwa akipokea ofa mbalimbali lakini amesisitiza anataka kupumzika.

Baada ya kupewa ubalozi huo wa heshima Klopp alisema:”LFC Foundation inafanya kazi nzuri katika jamii kuanzia ndani ya Jiji la Liverpool na nje ya hapa, nina furaha sana ya kuendelea kufanya kazi nao, pia nashukuru kwa kuchaguliwa kuwa balozi wa kwanza wa heshima wa taasisi hii.”

“Ninasubiri kuona nini tutafanya siku za usoni kwa sababu nina muda wa kutosha kwa sasa.”

Matt Parish, ambaye ni mtendaji mkuu wa LFC Foundation naye alisema: “Tuna furaha kuendelea kushirikiana na Klopp ambaye atakuwa balozo wa kwanza wa heshima katika taasisi yetu, amekuwa na akitusapoti sana katika nyanja mbalimbali na mapenzi yake na taasisi pamoja na Jiji la Liverpool ni makubwa sana.”

Taarifa ya Klopp kuwa balozi wa heshima wa taasisi hiyo zimekuja ikiwa ni siku mbili tu tangu iliporipotiwa amekataa ofa ya kuifundisha timu ya taifa ya Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live