Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool wakwea kileleni EPL kwa "Comeback" ya kibabe

IMG 6404.jpeg Liverpool wakishangilia bao la ushindi

Sun, 10 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Jana Jumamosi Uwanja wa Selhurst Park Jijini London.

Crystal Palace ilitangulia kwa bao la Jean-Philippe Mateta dakika ya 57 kwa penalti, kabla ya Mohamed Salah kuisawazishia Liverpool dakika ya 76, hilo likiwa bao lake la 200 tangu ajiunge na Wekundu hao wa Anfield

Bao la ushindi la Liverpool limefungwa na Harvey Elliott dakika ya 90 na ushei katika mchezo ambao Crystal Palace walimaliza pungufu kufuatia Jordan Ayew kuonyeshwa kadi mbili za njano na kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 75.

Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 37 katika mchezo wa 16 na kupanda kileleni ikiizidi pointi moja Arsenal wakati Crystal Palace inabaki na pointi 16 za mechi 16 nafasi ya 15.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live