Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool waichapa Leicester City Anfield

Liverpool Beat Leicester Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 2-1

Sat, 31 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majogoo wa Jiji, Timu ya Liverpool imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leicester City usiku wa Ijumaa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield.

Liverpool ilinufaika na makosa ya beki wa kati wa Leicester, Wout Faes aliyejifunga mabao yote mawili dakika za 38 na 45 baada ya kiungo Kiernan Dewsbury-Hall kutangulia kuwafungia wageni dakika ya nne.

Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 28 katika mchezo wa 16, ingawa inabaki nafasi ya sita wakati Leicester City inabaki na pointi zake 17 za mechi 17 nafasi ya 13.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live