Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool waichapa Everton Dabi ya Merseyside

IMG 6058.jpeg Mohammed Salah, Mfungaji wa Mabao ya Liverpool mchezo dhidi ya Everton

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WENYEJI, Liverpool FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Oktoba 21 Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.

Shujaa wa Liverpool alikuwa ni mshambuliaji wa Kimataifa wa Misri, Mohamed Salah aliyefunga mabao yote hayo, la kwanza kwa penalti dakika ya 75 na la pili dakika ya 90 akimalizia pasi ya nyota wa Uruguay, Darwin Nunez.

Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 20 na kusogea nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi moja mabingwa watetezi, Manchester City na Arsenal waliopo nafasi ya pili wakati Everton inabaki na pointi zake saba nafasi ya 16 ligi ya timu 18 baada ya wote kucheza mechi tisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live