Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool waichapa Brighton na kurudi kileleni EPL

Salah Late Winner Liverpool waichapa Brighton na kurudi kileleni EPL

Mon, 1 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majogoo wa Jiji, Liverpool wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Jumapili Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.

Brighton & Hove Albion walitangulia kwa bao la mshambuliaji Muingereza mwenye asili ya Ghana, Danny Welbeck dakika ya pili, kabla ya Liverpool kutoka nyuma kwa mabao ya washambuliaji wake hodari, Mcolombia Luis Díaz dakika ya 27 na Mmisri Mohamed Salah dakika ya 65.

Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 67 katika mchezo wa 29 na kuendelea kuongoza Ligi mbele ya Arsenal na Man City ambao walitoka sare ya bila kufungana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live