Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool waichapa Brentford Anfield

Liver Vs Brentford Liverpool waichapa Brentford Anfield

Sun, 7 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Liverpool FC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Brentford FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.

Bao pekee la Wekundu hao limefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Misri, Mohamed Salah dakika ya 13, akimalizia pasi ya beki Mholanzi, Virgil van Dijk.

Kwa ushindi huo, timu ya kocha Mjerumani, Jurgen Klopp inafikisha pointi 59 na kusogea nafasi ya tano, wakati Brentford inabaki na pointi zake 50 nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 34.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: