Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool waendelea kuifukuza Arsenal kileleni

Imago1037728965h 1280x853 Liverpool waendelea kuifukuza Arsenal kileleni

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Liverpool FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Sheffield United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Bramall Lane mjini Sheffield.

Mabao ya Liverpool yamefungwa na beki Mholanzi, Virgil van Dijk dakika ya 37 na kiungo wa Kimataifa wa Hungary, Dominik Szoboszlai dakika ya 90 na ushei.

Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 34, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na vinara, Arsenal baada ya wote kucheza mechi 15, wakati Sheffield United inaendelea kushika mkia na pointi zake tano za mechi 15 pia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live