Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool wababe haswa

P2021 12 16 Liverpool Newcastle 66 Wachezaji wa Liverpool wakipongezana

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Liverpool imeendelea na ubabe na kutoa vipigo kwenye kandanda ya Ligi Kuu England baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Newcastle United mtanange uliopigwa dimba la Anfield.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Misri pia Mohamed Salah ameendelea kuwa na urafiki na goli baada ya kufunga goli la 22 kwenye msimu huu ikiwa ni rekodi ya aina yake, mabao mengine yakafungwa na Diogo Jota na Trent Alexander Arnold.

Ushindi wa Majogoo wa Jiji la Merseyside Liverpool wanafuta pengo dhidi ya kinara Manchester City ambayo ilishinda dhidi ya Leeds United.

Hata hivyo, Liverpool ni miongoni mwa klabu ambazo haziathirika sana na maambukizi ya virusi vya Covid-19 kwani wachezaji wawili pekee walikosa mchezo huo akiwemo Virgil van Dijk na Fabinho.

Bao la Newcastle United likifungwa na Jonjo Shelvey ambao sasa wanabakia nafasi ya 19 kwenye msimamo wa EPL.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live