Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool waanza na ushindi Uropa Ligi

SEI172662904 Wachezaji wa Liverpool wakipongezana

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Liverpool imetoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, LASK usiku wa jana katika mchezo wa Kundi E UEFA Europa League Uwanja wa Raiffeisen Arena mjini Linz nchini Austria.

Florian Flecker alianza kuifungia LASK dakika ya 14, kabla ya Liverpool kuzinduka na mabao ya Darwin Nunez dakika ya 56, Luis Diaz dakika ya 63 na Mohamed Salah dakika ya 88.

Mechi nyingine ya Kundi E jana, wenyeji Union Saint-Gilloise walilazimishwa sare ya 1-1 na Toulouse ya Ufaransa Uwanja wa Lotto Park mjini Brussel, Ubelgiji

Chanzo: www.tanzaniaweb.live