Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool waambiwa uzeni Salah Pauni 100 milioni

Mohammed Salah 2 Goals.jpeg Winga wa Liverpool, Mohammed Salah

Sun, 16 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Straika wa zamani wa Liverpool, Emile Heskey amewaambia mabosi wa miamba hiyo ya Anfield kwamba wanaweza kuchagua kupiga pesa kiasi cha Pauni 100 milioni kwa kumuuza supastaa wao, Mohamed Salah kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya.

Mo Salah amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa kwenye kikosi hicho cha Liverpool kitakachokuwa chini ya kocha mpya Arne Slot baada ya Jurgen Klopp kuondoka, hivyo ni vyema kama timu ikija na pesa nyingi kiasi hicho staa huyo akauzwa kuliko kusubiri aondoke bure.

Winga huyo wa kimataifa wa Misri, Mo Salah alifunga mabao 25 na kuasisti 14 msimu uliopita na kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kunatazamiwa kuwapo na ofa za kutoka kwa klabu za Saudi Arabia zinazohitaji huduma ya mchezaji huyo.

Mo Salah amefunga mabao 211 tangu alipotua kwenye klabu hiyo ya Liverpool akitokea AS Roma kwa ada ya Pauni 36.9 milioni mwaka 2017. Liverpool iligomea ofa ya Pauni 150 milioni mwaka jana baada ya klabu moja ya Saudi Pro League kuvamia Anfield kuhitaji saini yake.

Na sasa, Heskey anaamini staa huyo licha ya kubakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake huko Anfield, bado timu hiyo inaweza kupiga pesa ndefu kwenye mauzo yake na kupata faida.

Akizungumza na OLBG , staa huyo aliyewahi kuichezea pia Aston Villa, Heskey alisema: “Kumuuza Mohamed Salah kwenye dirisha hili ni mjadala mzuri, nadhani Liverpool bado inaweza kupata Pauni 100 milioni kwenye mauzo yake. Ni uamuzi mgumu kwa sababu ni mchezaji mwenye uwezo wa kufunga mabao 20 na zaidi kwa msimu.”

Heskey anaamini Liverpool inaweza kumuuza Mo Salah na kisha ikaenda kumsajili winga wa Crystal Palace, Michael Olise.

Hata hivyo, huduma ya Olise itahitaji vita kubwa kutokana na klabu za Chelsea na Manchester United nazo kuhitaji huduma yake.

Chanzo: Mwanaspoti