Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool vs Real Madrid UEFA, PSG watupwa kwa Bayern Munich

Liver Vs Real Madrid Liverpool wamekuwa na rekodi mbaya kwa miaka ya hivi karibuni mbele ya Real Madrid

Mon, 7 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa mara 6 wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, Timu ya Liverpool wamepangwa kucheza na Real Madrid katika hatua ya 16 Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Mechi hiyo ni kumbu kumbu ya Fainali ya msimu uliopita zilizopigwa Jijini Paris nchini Ufaransa ambapo vijana wa Carlo Ancelotti walibeba taji lao la 14 kwa Michuano ya Ulaya baada ya ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Vinicious.

Mechi za hatua ya 16 bora zitapigwa;

Mechi za mkondo wa kwanza zitapigwa katikati ya wiki ya Februari 14/15 na Februari 21/22 mwakani na mechi za marudiano zitakuwa Machi 7/8 na 14/15 mwakani.

Droo ya kupangwa kwa mechi hizo imefanyika mchana wa leo Novemba 7 na mechi nyingine ni kama ifuatavyo;

RB Leipzig vs. Man City

Club Bruges vs. Benfica

Liverpool vs. Real Madrid

Eintracht Frankfurt vs. Napoli

AC Milan vs. Tottenham

Dortmund vs. Chelsea

Inter Milan vs. FC Porto

PSG vs. Bayern Munich

Chanzo: www.tanzaniaweb.live