Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool vs Chelsea, namba zinawakataa Liverpool

Gakpo Anfield Mshambualiaji wa Liverpool, Cody Mathès Gakpo akimtoka kiungo wa Chelsea

Sat, 21 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

(LIVERPOOL)

Liverpool wanaweza kuifikia record yao ya mwaka 1953, ambayo ni ya kupoteza mechi tatu za mwanzo wa mwaka katika ligi, hii ni kama watapoteza dhidi ya The blues leo.

Liverpool wameruhusu bao katika michezo yao nane iliyopita ya premier league, endapo wataruhusu bao kwenye mchezo wa leo, watakuwa waruhusu bao katika michezo tisa mfululizo ya premier league kwa mara ya kwanza tangu 2016 Mei hadi Oktoba.

Liverpool iwapo hawatoshinda kwenye mchezo wa hii leo, watakuwa wamepata points chache zaidi (28) katika nusu ya msimu wa premier league kwa mara ya kwanza tangu 2014-15.

Mohamed Salah amehusika katika mabao manne dhidi ya Chelsea kwenye michezo mitano ya premier league katika dimba la Anfield.

michezo 5

mabao 3

pasi ya bao 1

(CHELSEA)

Chelsea wamefunga mabao 22 mpaka sasa katika premier league, ni mabao yao machache zaiidi kuwahi kuyafunga katika nusu ya msimu wa premier league tangu 1995-96.

Chelsea endapo wataibuka na ushindi dhidi ya Liverpool leo, kocha wao Graham Potter atakuwa kocha watatu wa kiingereza kuwafunga Liverpool kwenye ligi katika dimba la Anfield akiwa na klabu mbili tofauti (Brighton na Chelsea), baada ya Kevin Keegan na Ron Atkinson.

Chelsea wamepata ushindi katika mchezo mmoja pekee kati ya michezo yao mitano iliyopita ya premier league ambayo muamuzi wa Kati alikuwa ni Michael Oliver, wamefungwa michezo mitatu na kutoa sare mmoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live