Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool ushindi 100% UEFA

P2021 11 24 Liverpool Porto 39 Kiungo wa Liverpool, Thiago Alcantara akishangilia goli lake dhidi ya Porto

Thu, 25 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majogoo wa Jiji, Timu ya Liverpool jana usiku wameedeleza wimbi la ushindi baada ya kuichapa Porto mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi B, Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Anfield.

Mabao ya Liverpool jana yamefungwa na Thiago Alcantara kwa shuti kali la dakika ya 52 na Mohamed Salah dakika ya 70 na ushindi huo ni mwendelezo wa rekodi nzuri ya kushinda mechi zake zote.

Katika hatua ya makundi Liverpool mpaka sasa imeshacheza michezo mitanpo na kushinda yote.

Liverpool sasa inafikisha pointi 15 na kuendelea kuongoza kundi hilo, huku ikiwa imeshakata tiketi ya hatua ya 16 bora, ikifuatiwa kwa mbali na Porto pointi tano, AC Milan nne sawa na Atletico Madrid baada ya wote kucheza mechi tano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live