Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool ubingwa ndio basi tena, wachapika goli

IMG 6822.jpeg Liverpool baada ya kipigo cha bao 2-0 wamepoteza matumaini ya Ubingwa wa EPL

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Everton wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mahasimu wao, Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Goodison Park, Liverpool.

Mabao yaliyoikata kilimi Liverpool yamefumgwa na Waingereza, beki Jarrad Branthwaite dakika ya 27 na mshambuliaji Dominic Calvert-Lewin dakika ya 58.

Kwa ushindi huo, Everton inafikisha pointi 33 na kusogea nafasi ya 16, wakati Liverpool inabaki na pointi zake 74 nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na Arsenal baada ya wote kucheza mechi 34.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live