Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool njia nyeupe kwa Kimmich

Joshua Kimmich Furaha Joshua Kimmich

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Njia ya Liverpool kuipata huduma ya beki wa Bayern Munich, Joshua Kimmich katika dirisha hili huenda ukakamilika baada ya beki huyo kuonyesha nia ya kutaka kuondoka licha ya kupewa ofa ya kusaini mkataba mpya.

Kimmich mwenye umri wa miaka 29, mkataba wake unamalizika mwaka 2025 na Bayern inataka kumuuza ili asiondoke bure mwisho wa msimu ujao.

Mbali ya Liverpool, staa huyu pia anawindwa na Manchester City, Real Madrid na Barcelona ingawa nyingi kati ya hizo zinaonekana kutaka kusubiri hadi mwisho wa msimu ujao ndio kumsajili.

Taarifa zinaeleza kwamba Bayern inahitaji zaidi ya Pauni 50 milioni ili kumuuza ingawa kuendelea kuwa naye hadi msimu ujao inaweza kushusha bei yake kwa sababu mkataba wake utakuwa unaelekea ukingoni.

Msimu uliopita alicheza mechi 45 za michuano yote, amefunga mabao mawili na kutoa asisti kumi na moja.

Chanzo: Mwanaspoti