Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

“Liverpool ndiyo wapinzani wetu wa karibu” Guardiola

Skysports Klopp Guardiola Pep 4436355 Jurgen Klopp na Pep Guardiola wanakutana Jumapili hii

Sat, 15 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anaamini kuwa pamoja na kuwa Liverpool ilianza vibaya msimu huu wa mashindano na kushika nafasi ya kumi kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, bado ndio wapinzani wao wa karibu.

Guardiola amesema hayo wakati akiteta na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo utakaomkutanisha na mpinzani wake Jurgen Klopp siku ya Jumapili Anfield kukiwa na tofauti ya pointi 13 baina yao.

Licha ya matokeo hayo mabaya, Guardiola alisema anaamini mpinzani mkubwa wa Man City ni Liverpool, akisema upinzani utaendelea kuwa hivyo.

Hata hivyo, kocha huyo ameeleza kuwa kama swali hilo lingeulizwa wakati Ligi inaelekea ukingoni (zingebakia mechi 10) angesema Liverpool hawatakuwa juu kwenye msimamo lakini kwa sasa bado ni wapinzani wakubwa na watarudi kwenye ubora mkubwa.

Huenda kauli ya Pep ikawa kejeli kwani tangia alipofika Etihad ameshinda mara nne na Klopp akishinda mara moja kwenye msimu wa ‪2019-20‬.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live