Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool majanga tu huko

Virgil Van Dijk Complains To The Referee Beki wa Liverpool, Virgil Van Dijk

Fri, 6 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Liverpool, Virgil van Dijk atafanyiwa vipimo na madaktari Jurgen Klopp akihofia hali yake baada ya kupata majeraha ya misuli ya paja.

Beki huyo hakuendelea na mechi ya Ligi Kuu England baada ya kupata majeraha hayo, Liverpool ikichezea kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Brentford wikiendi iliyopita.

Mholanzi huyo aliumia kipindi cha kwanza tu cha mchezo huo baada ya hapo alipewa ushauri wa kuonana na daktari kwa ajili ya vipimo zaidi taarifa zimeripoti. Liverpoo imepata hofu huenda Van Dijk atakuwa nje ya dimba kwa mda mrefu akijiuguza lakini Klopp amejipa matumaini jeraha la beki huyo tegemeo kwenye kikosi sio kubwa, kama taarifa zilivyoripoti.

Akizungumza na waandishi wa habari Klopp amesema Van Dijk alipata maumivu ya misuli ya paja, lakini anaendelea vizuri na hajapaniki baada ya kuumia.

"Van Dijk alijisikia maumivu, lakini yupo sawa hajakuwa na hofu, baada ya kuisikia maumivu niliogopa nfio maana nikamtoa haraka, madaktari walifurahia maamuzi yangu, tulijawa hofu tatizo lisije kuwa kubwa zaidi,"alisema Klopp.

Kwasasa Liverpool ipo mbioni kumrudisha beki wao Billy Billy Koumetio anayekipiga kwa mkopo Rapid Vienna na inayosemekana atachukuwa nafasi ya Van Dijk kipindi hiki ambacho atakuwa nje ya dimba.

Aidha Klopp ana wachezaji wengine wanaocheza nafasi ya Van Dijk kama Joel Matip, Ibrahima Konate, Joe Gomez na Nat Phillips kwasababu klabu hiyo haina mpango wa kusajili beki dirisha dogo la usajili.

Liverpool imefanya usajili wa mchezaji mmoja tu Cody Gakpo aliyegharimu kitita cha Pauni 44 milioni akitokea PSV. Awali winga huyo alikuwa akiwaniwa na Manchester United hata hivyo usajili ukabuma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live