Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool kuwakosa Thiago, Arnold dhidi ya Man City Jumapili

Pjimage (23) Wachezaji wa Liverpool watakaoukosa mchezo dhidi ya Man City

Fri, 1 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Kulia wa Liverpool, Trent Alexander Arnold na kiungo Thiago Alcantara watakosekana katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Mabingwa watetezi Manchester City.

Beki Alexander Arnold hakujumuishwa katika kikosi cha jumapili kutokana na maumivu ya misuli yanayomsumbua wakati Thiago yeye anasumbuliwa na maumivu katika kiazi cha mguu, maumivu aliyoyapata katika mechi dhidi ya Crystal Palace.

Wachezaji wote hao walikosekana katika ushindi wa magoli 5-1 dhidi ya Porto, ugenini katika mechi ya Ligi ya Mabingwa.

Akizungumzia utimamu wa wachezaji hao, Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema; "Hakuna jipya ila tu niweze kusema hatutakuwa nao katika mchezo dhidi ya Man City, lakini natarajia tutakua nao wote baada ya mapumziko kupisha mechi za Mataifa"

Lakini tuna kikosi kizuri kwa hiyo bado tuna namna na tunahitajika kuwatumia waliopo" amesisitiza Klopp

Liverpool wanakwenda katika mchezo dhidi ya Manchester City ikiwa ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo EPL, na wanategemea kutumia faida yao ya kuongoza kwa tofauti ya alama moja katika kilele cha msimamo wa Ligi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live