Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool kutibua harakati za Ubingwa wa Arsenal leo?

Liver Vs Gunners Liverpool kutibua harakati za Ubingwa wa Arsenal leo?

Sun, 9 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Liverpool leo watashuka dimbani kumenyana na klabu ya Arsenal katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza huku majogoo hao wa Anfield wakiwa katika dimba lao la nyumbani na ndipo maswali mengi yanaibuka kama wataweza kuishangaza klabu ya Arsenal.

Liverpool wamekua chini ya kiwango zaidi msimu huu mpaka sasa wakishika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama zao 43, Hii inaonesha namna klabu hiyo inapitia kipindi kigumu msimu huu na wanakwenda kukutana na Arsenal ambao wamekua kwenye kiwango bora sana msimu huu.

Klabu ya Liverpool licha ya kutofanya vizuri msimu huu wamekua wakipata matokeo mazuri kwenye dimba lao la Anfield tena dhidi ya vigogo, Kwani vilabu kama Manchester City na Man United vilipokea kipigo kwenye dimba hilo hivo matumaini makubwa kuelkea mchezo huo ni huenda klabu hiyo ikafanya maajabu kwenye dimba lao la nyumbani.

Klabu ya Arsenal wanakwenda kwenye mchezo dhidi ya majogoo wakitambua kabisa dimba la Anfield sio uwanja mwepesi kabisa, Hivo watakwenda na tahadhari kubwa licha ya kua kwenye ubora mkubwa msimu huu kwani uwanja huo umeshatoa adhabu kwa vigogo ndani ya msimu huu.

Liverpool wametoka kupokea kichapo kizito wikiendi iliyomalizika dhidi ya klabu ya Manchester City na mipango yao bado ni kuwania nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa ulaya, Hivo watahitaji kupata matokeo katika mchezo wa leo ili waweze kurudi kwenye njia hii ni wazi itafanya mchezo kua mkali kwani Arsenal nao wanautolea macho mchezo kwajili ya kujiwekea mazingira mazuri kwenye mbio za ubingwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live