Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool kupindua meza kwa Madrid leo?

Madrid Vs Liver 2nd Leg Liverpool kupindua meza kwa Madrid leo?

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mechi 2 za kuhitimisha hatua ya 16 bora zinaendelea tena leo Machi 15, 2023.

REAL MADRID vs LIVERPOOL Uwanja : Santiago Bernabeu Muda saa: 5:00 usiku

Mabingwa watetezi, Real Madrid watakuwa wenyeji wa Liverpool katika dimba la Santiago Bernabeu wakiwa na uongozi mnono wa tofauti ya magoli matatu baada ya ushindi wa 5-2 kwenye raundi ya kwanza.

Real Madrid imeshinda mechi 6 kati ya mechi 7 zilizopita dhidi ya Liverpool (sare moja) ukiwemo ushindi wa 1-0 kwenye fainali ya #UCL msimu uliopita ambapo miamba hiyo ya Uhispania ilitwaa ubingwa wa Ulaya kwa mara ya 14.

Real Madrid itakuwa inacheza mechi ya 300 kwenye Ligi ya Mabingwa ikiwa ndio klabu pekee kufikia idadi hiyo ya mechi katika historia ya UEFA Champions League.

Liverpool ina kibarua cha kupindua meza kwa tofauti ya mabao matatu kwa mara nyingine tena ikiwa ndio moja ya timu chache kuwahi kupindua matokeo ya aina hiyo.

Liverpool ilifanya hivyo dhidi ya mahasimu wa Real Madrid, FC Barcelona mnamo Mei 8, 2019 wakitoka nyuma 3-0 na kushinda 4-0 kwenye mchezo wa marudiano katika dimba la Anfield.

Magoli mawili ya Giorginio Wijnaldum usiku huo na mawili kutoka kwa Divock Origi bao moja likichagizwa na pasi janja ya Trent Alexander Arnold kutoka mpira wa kona yaliwapeleka Majogoo FAINALI.

Hadithi ya leo ni tofauti kidogo kwa Majogo kwa kuwa watatakiwa kufanya hiyo ‘Remontada’ wakiwa mbali na dimba lao la Anfield, safari hii wakihitaji kupindua meza huko Santiago Bernabeu, Madrid.

Mchezo mwingine utakaopigwa leo;

23:00 || NAPOLI vs EINTRACHT FRANKFURT

Chanzo: www.tanzaniaweb.live