Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool inamtaka Mbappe

Kylian Mbappe Fiert Win Kylian Mbappe

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Habari ndo hiyo. Liverpool bado inaamini kwamba itakamilisha dili lake litakaloshtua wengi la kunasa saini ya Kylian Mbappe baada ya kuzungumza na kambi ya mchezaji huyo kwa miaka sita, imeelezwa.

Hatima ya Mbappe huko kwenye kikosi cha Paris Saint-Germain ipo kwenye mashaka makubwa baada ya kugomea kusaini mkataba mpya wakati wa majira ya kiangazi yaliyopita na dili lake la sasa litafika tamati mwisho wa msimu huu.

Klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia iliipelekea PSG ofa ya Pauni 257 milioni kumsajili Mbappe kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi, lakini mchezaji huyo hakushawishika.

Real Madrid ilionekana ni mahali ambako mchezaji huyo anataka kwenda, lakini Liverpool wameibuka kwa kasi wakiamini wanaweza kumnasa.

Mbappe kwa sasa amebaki mwenyewe kwenye kikosi cha PSG baada ya mastaa wenzake Neymar na Lionel Messi - wote kuachana na timu hiyo kwenye dirisha lililopita mmoja akienda Saudi Arabia na mwingine Marekani.

Mbappe anafanya vizuri, lakini bado hajasaini mkataba mpya na itakapofika Januari atakuwa amebakiza miezi sita tu, ambayo itampa uhuru wa kusaini mkataba wa awali na klabu yoyote ya ng’ambo ili kujiunga nayo bure mwishoni mwa msimu.

Tangu alipojiunga na PSG, Mbappe amefunga mabao 224 katika mechi 272. Msimu huu amefunga mabao 12 katika mechi 12 katika mechi za ligi na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Liverpool wanahitaji saini yake wakati wakijiandaa kumpoteza Mohamed Salah anayewindwa na timu za Saudi Arabia.

Chanzo: Mwanaspoti