Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool hao nusu Fainali, Uso kwa uso na Man City Wembley

Dogo Jotta Semi Final Diogo Jota, akishangilia goli la ushindi

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Liverpool imeendelea kukimbiza ndoto yake ya kubeba mataji manne msimu huu wa mashindano baada ya kushinda kibabe goli 1-0 dhidi ya Nottingham Forest katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA.

Sasa Liverpool itacheza na Manchester City katika hatua hiyo mchezo wa nusu fainali ya Kombe hilo uwanja wa Wembley.

Bao pekee kwa Majogoo wa Jiji la Merseyside limefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno Diogo Jota, likiwa ni bao la 19 kwake msimu huu.

Kama mambo yatakuwa poa kwa Liverpool, kuna uwezekano wa msimu huu kuondoka na mataji manne ingawa inahitaji juhudi na bahati pia.

Tayari wameshinda Kombe la Carabao dhidi ya Chelsea, wako nafasi ya pili kwenye msimamo wa EPL, wako hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo, Nottingham Forest wameondoka uwanjani kama mashujaa kutokana na ubora mkubwa waliouonyesha kwenye mechi hiyo wakipoteza nafasi kadhaa ikiwemo ya Philip Zinckernagel na Yatea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live