Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool haikamatiki EPL, Salah kama kawaida yake

Pjimage (42) Washambuliaji wa Liverpool

Sat, 16 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majogoo wa Jiji Liverpool wamemkaribisha kocha mpya wa Watford, Claudio Ranieri kwa kipigo cha magoli 5-0.

Ranieri ambae alikuwa anaongoza mchezo wake wa kwanza kama kocha wa Watford, tangu achukue kibarua hicho wiki mbili zilizopita, alijikuta akikumbana na hasira za washambuliaji watatu wa liverpool waliopeleka kilio ndani ya uwanja wa Vicarage road.

Roberto Firmino ambae mwanzo wa msimu alianza kwa majeruhi, alipata nafasi ya kuanza katika kikosi cha leo na akafunga magoli matatu (Hat-trick).

Magoli mengine ya Liverpool yamefungwa na Sadio Mane na mchezaji hatari kwa sasa Mohamed Salah.

Ushindi huo unawafikisha Liverpool kileleni mwa msimamo wa EPL, wakijikusanyia alama 18, wakiwa wameshacheza michezo 8.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live