Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool bado wanaitaka Top Four

Diogo Jota Score Last Winning.jpeg Diogo Jota alifunga bao la ushindi kwa Liverpool

Mon, 1 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Liverpool bado hawajaikatia tamaa nafasi kua kwenye timu nne za juu ambazo zitashiriki ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao baada ya kufanikiwa kushinda mchezo wake dhidi ya Tottenham katika dimba la Anfield jana Jumapili.

Liverpool wamefanikiwa kupanda mpaka nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuichapa klabu ya Tottenham Hotspurs kwa mabao 4-3 na kufufua rasmi matumaini ya kumaliza kwenye nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Vijogoo wa Anfield walifanikiwa kupata mabao matatu ndani ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Curtis Jones, Luiz Diaz, na Mohamed Salah huku Tottenham nao wakipata bao moja kupitia kwa Harry Kane na mchezo kwenda mapumziko Spurs wakiwa nyuma kwa mabao 3-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa Tottenham wakionekana kuhitaji kusawazisha mabao ambayo wametanguliwa kutokana na kasi ambayo walianza nayo na ndivyo ilivyokua kwani dakika ya 77 Heung Ming Son aliipatia bao la pili Spurs kabla ya Richarlison kusawazisha dakika za nyongeza na kufanya ubao kusomeka 3-3, Lakini Diogo Jota dakika ya 94 aliipatia Liverpool bao la nne na kuhakikisha alama tatu zinabaki Anfield.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: