Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool, Man City hapatoshi mbio za Ubingwa EPL

Liver Leeds Liverpool waliibuka na ushindi wa magoli 6-0

Thu, 24 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Liverpool imeibuka na ushindi mnono wa goli 6-0 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa dimba la Anfield Jumatano Februari 23, ukiwa ni mchezo kiporo.

Ushindi wa Majogoo wa Jiji la Merseyside unaifanya kupunguza pengo la pointi kutoka sita mpaka tatu. Liverpool imecheza mechi sawa (26) na vinara Manchester City.

Magoli ya Liverpool yamefungwa na Mohamed Salah mawili yote kwa penati, beki Joel Matip, Sadio Mane mawili kisha goli la kichwa la mlinzi wa kati wa Uholanzi Virgil van dijk akimalizia mpira wa kona wa Robertson.

Ushindi huo unaweza kuwapa nguvu Liverpool ambao Jumapili watacheza na Chelsea Fainali ya Kombe la Carabao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live