Majogoo wa Jiji, Timu ya Liverpool wamefanikiwa kubeba ndoo yao ya pili msimu huu baada ya kuibuka na ushindi wa Penati 5-6 dhidi ya Chelsea katika Dimba la Wembley.
Mchezo huo wa Fainali baina ya vigogo hao ulikuwa wa piga nikupige tangu dakika ya Kwanza ya mchezo huku Liverpool wakianza kwa kasi dakika 15 za kwanza wakipeleka mashambulizi ya hatari kupitia Winga wao Luis Diaz.
Dakika 120 zilikamilika pasipo timu yoyote kupata bao na katika changamoto ya mikwaju ya penati Chelsea walikosa mikwaju miwili kupitia kwa Azpilicueta na Mount huku Sadio Mane akikosa kwa upande wa Liver.
Mara ya Mwisho kwa Liverpool kubeba Kombe la FA ni mwaka 2006, na May 28 mwaka huu anakutana na Real Madrid katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.