Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool Kwenye Rekodi Mpya UCL

Inter Milan V Liverpool2 Liverpool iliibuka na ushindi wa magoli 2-0 usikuwa Jumatano vs Inter

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Liverpool imeingia kwenye rekodi ya kushinda michezo saba mfululizo katika Ligi ya Mabingwa kwa vilabu kutoka Uingereza baada ya kuifunga Inter Milan bao 2-0 siku ya Jumatano usiku ikiwa ni hatua ya 16 bora.

Barcelona, Real Madrid na Bayern Munich walikuwa tayari wamefanya hivyo Liverpool wanakuja kwenye hatua hiyo baada ya kushinda michezo yote 6 ya makundi wakimaliza juu kwenye kundi B na kuwa timu ya kwanza ya Premier League kuweka rekodi hiyo.

The Reds ndiyo timu pekee yenye mafanikio zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa wakiwa wameshinda ubingwa huo mara sita wakati mataji manne kati ya hayo manne ni wakati michuano hiyo inajulikana kama European Cup (1976-77, 1977-78,1980-81 na 1983-84) na wakati Mashindano yamebadilishwa jina ilikuwa ni mwaka (2004-05, 2018-19).

Liverpool walifuzu kucheza michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza msimu wa 1964-65 na waliweza kufika mpaka nusu fainali ya michuano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live