Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool, Chelsea chali

Liverpool Pic Liverpool, Chelsea chali

Tue, 13 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Timu za Ligi Kuu England zimeendelea kupasha ili wachezaji wajiweke fiti kabla ya ligi kuendelea baada ya michuano ya Kombe la Dunia ambayo itafikia tamati Desema 18, na Chelsea na Liverpool zilishuka dimbani kucheza michezo ya kirafiki, lakini zikachezea kichapo.

Liverpool ilipokea kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Lyon huku nyota wake Mohamed Salah akikosa penalti katika mchezo wa Dubai Super Cup.

Katika mchezo huo nyota wa zamani wa Arsenal, Alexandre Lacazette alifungia Lyon mabao mawili. Liverpool ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya kwanza lililowekwa kimiani na Fabio Carvalho.

Liverpool ingekuwa mbele kwa mabao 2-0 kipindi cha kwanza, lakini Salah alikosa penalti dakika ya 14.

Vilevile Liverpool ilipata pigo baada ya Harvey Elliott kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo.

Kila baada ya mechi michuano hiyo ya Dubai Super Cup inakuwa na changamoto ya mikwaju ya penalti pamoja na pointi ya bonasi kama ofa. Baada ya kipigo cha mabao 3-1 Liverpool ilipoteza tena kwa mikwaju ya penalti 3-5 dhidi ya Lyon.

Mechi inayofuata ya Liverpool itakuwa dhidi ya AC Milan.

Chelsea 0- 1 Aston Villa

Vijana wa kocha Graham Potter walipokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Aston Vila, nyota wao Armando Broja akipata majeraha kwenye mchezo huo.

Straika huyo alianza mechi hiyo iliyochezwa Dubai lakini akashindwa kuendelea na kuondolewa dakika ya 25 tu baada ya kugongana na beki wa Villa, Ezri Konsa.

Nafasi yake ikachukuliwa na Dion Joseph Rankine. Cheslea itacheza mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Bourthemouth Desemba 27. Mastaa Mason Mount, Raheem Sterling na Conor Gallagher wapo mbioni kuungana nao

Chanzo: Mwanaspoti