Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lionel Messi, kweli Mungu humuinua anaejishusha

MESSI KURA Lionel Messi, kweli mungu humuinua anaejishusha

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Neno linatufundisha kujishusha kwa sababu mtu anayejishusha siku zote Mungu humuinua sana (Yakobo 4:10).

Hiki ndicho alichokifanya Lionel Messi, nyota bora zaidi kuwahi kutokea kwenye soka, kwa mujibu wa wabobezi wengi.

Messi ametangazwa kuwa mchezaji bora wa dunia wa FIFA juzi Jumatatu, baada ya kushinda tuzo inayoitwa The Best.

Mshindi wa tuzo hii hupatikana kwa kura ambazo hupigwa na manahodha na makocha wa timu za taifa duniani.

Messi mwenyewe ni nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, angeweza kujipigia kura lakini hakufanya hivyo.

Badala yake akajishusha na kuwapigia kura wengine kabisa kama akionesha kukubali uwezo unaooneshwa na wenzake

Lakini Mungu akamuinua na kumpa ushindi kwa kupigiwa kura na watu wengine. Messi is infinity!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live