Unaambiwa tangu ajiunge na Inter Miami, Lionel Messi amekuwa akilindwa na mlinzi binafsi dhidi ya usumbufu ambao unaweza kutokea nje ya uwanja.
Mlinzi huyo (bodyguard) anayefahamika kwa jina la Yassine Cheuko ni Mwanajeshi mstaafu wa Jeshi la Wanamaji la Marekani
Cheuko ambaye ni mtaalamu wa sanaa za kijeshi, ndondi na taekwondo alipigana vita vya Iraq na Afghanistan kabla ya kustaafu na kuamua kuwa mkufunzi na mchezaji wa ngumi za MMA na Taekwondo.
Cheuko ambaye ameajiriwa na mmiliki mwenza wa klabu ya Inter Miami David Beckham kwa ajili ya kumwekea ulinzi mshindi huyo mara 7 wa Ballon d'or amekuwa akionekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa na Muargentina huyo kila mahali kuhakikisha usalama wake.