Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lionel Messi ajitetea kukosekana katika mechi ya kirafiki ya Hong Kong

Lionel Messi Ajitetea Kukosekana Katika Mechi Ya Kirafiki Ya Hong Kong Lionel Messi ajitetea kukosekana katika mechi ya kirafiki ya Hong Kong

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Mshambuliaji Lionel Messi amejitetea baada ya mashabiki wa huko Hong Kong kuwazomea Inter Miami kwa sababu alikosa mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya.

Inter ilishinda Ligi XI 4-1 mbele ya karibu mashabiki 40,000 siku ya Jumapili, huku nahodha wa Argentina Messi akiachwa kwenye benchi kwa sababu ya tatizo la misuli ya paja.

Serikali ya Hong Kong ilisema Messi alipewa kandarasi ya kucheza angalau dakika 45.

“Siku zote huwa natamani kucheza, hasa katika michezo hii ambayo tunasafiri mbali na watu wanataka kuona michezo yetu,” alisema.

"Kwa bahati mbaya hii hutokea katika soka. Katika mchezo wowote inaweza kutokea kwamba huwezi kucheza.

"Natumai tunaweza kurudi na kucheza mchezo huko Hong Kong."

Wafuasi katika umati wa karibu wa watu 38,323 katika Uwanja wa Hong Kong walilipa zaidi ya HK$1,000 (£101) kwa tikiti.

Chanzo: Bbc