Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lionel Ateba kimeeleweka Simba SC, kuwavaa Singida Big Stars

Lionel Ateba Kimeeleweka Simba SC,  Kuwavaa Singida Big Stars.png Lionel Ateba kimeeleweka Simba SC, kuwavaa Singida Big Stars

Tue, 20 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rasmi mshambuliaji mpya wa Simba, Lionel Ateba ataanza kuitumikia timu hiyo, katika michez ijayo ya Ligi Kuu Bara baada ya kupata vibali.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa mshambuliaji amekamilisha taratibu zote zinazohitajika ikiwemo kupata vibali vya kucheza soka na kuishia nchini na ITC.

Straika huyo tayari ameanza kujumuisha katika mipango ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Fadlu Davids kuelekea michezo ijayo ya ligi kuu ambapo wikiendi hii, Agosti 25, 2024, watakuwa nyumbani kuwakabili Singida Big Stars.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live