Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liogope anyoosha mikono kwa Azam FC

Azam Dodoma Liogope anyoosha mikono kwa Azam FC

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha msaidizi wa Dodoma Jiji, Kassim Liogope amesema sare waliyopata dhidi ya Azam (jana) ilitokana na namna ambavyo aliwasoma wapinzani wake hao na kugundua inatumia viungo wengi katika mechi zao.

Dodoma Jiji na Azam zilitoka 0-0 mchezo uliochezwa jana katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Liogope amesema baada ya kugundua hilo, katika mechi yao waliingia wakiwa na viungo watano jambo ambalo liliwasaidia kuikabili timu ya Azam.

"Malengo yalikuwa pointi tatu lakina hata hii sio haba, wapinzani wetu tuligundua wana viungo wengi ambapo wanaongezewa nguvu na mabeki wa pembeni pale timu inaposhambulia," amesema Liogope na kuonmgeza;

"Kipindi cha pili wetu walifanya mabadiliko ya kuingiza washambuliaji wawili lakini bado tulipambana nao kuhakikisha tunakuwa bora."

Liogope ameongeza akisema waliwabana wapinzani wao kwenye eneo la kiungo hali ambayo iliwalazimu kutumia mbinu ya kupiga mipira mirefu.

"Unajua baada ya kuwabana walikosa njia ya kupita na wakaanza kutumia mbinu ya kupiga mipira mirefu, hawakufanikiwa kwa sababu mabeki wetu wa pembeni walikuwa bora zaidi," amesema Liogope.

Matokeo ya juzi yameifanya Dodoma Jiji kuongeza pointi moja na kufikisha pointi tano baada ya mechi tano na kupanda kwa nafasi moja kutoka ya nane hadi ya saba, huku Azam ikipanda hadi kileleni mwa msimamo ikifikisha pointi 10 na kuiengua Yanga ambayo jioni hii ya leo itashuka uwanja jijini Mbeya kuvaana na Ihefu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live