Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lini mtampa Mzize heshima yake?

Clement Mzize Clementinho Straika wa Yanga, Clement Mzize

Tue, 6 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama unajijua haufahamu soka vizuri usipoteze muda kusoma hili andiko. Tafuta kazi zingine ukafanye. Leo naandika na kumzungumzia Mzize kwa ajili ya “Watu wa mpira”

Nawasikia mtaani huko mnasema Mzize anazingua, mara ooh! Mzize hafai. Leo nataka tuongee soka, leo ni mwendo wa ‘Facts after Facts’ nataka baada ya hili andiko heshima ya Mzize ikae mahala pake.

Sasa nisikilizeni

Mwaka 2019, Clement Mzize was a nobody. Hakuna ambae alikua anamjua. Hapa naongelea miaka minne nyuma kipindi yupo Iringa anapiga kazi yake ya kuendesha boda.

Msimu wa 2020-2021, Mzize akiwa mjini alishiriki mashindano ya Under20 Ligi kuu na kuwa mfungaji bora. Hakubahatisha, aliwatesa sana vijana wenzake.

Msimu wa 2022-2023 Mzize alipandishwa senior team, Yanga ikiwa chini ya Nabi Mzize alianza kupata nafasi. Alicheza mechi 21, alifunga bao 05, assists 02

Msimu wa 2023-2024, Mzize alicheza mechi 28, alifunga bao 06, assists 07. Alikua na mchango wa GA ( Goals & assists) - 14

Mpaka hapa tunaenda sawa?

Nmesema leo ni ‘facts after facts’ — Asikimbie mtu. Naomba niendelee na mada.

Clement Mzize, msimu huu ulioisha ndio msimu wake bora tangu aanze kucheza ligi kuu. Amechukua kombe la FA, amekua top-scorer FA, amebeba ubingwa wa ligi kuu, amefunga bao nyingi na kutoa assists nyingi kuliko misimu ya nyuma. Je kuna mtu anaipinga hii fact?

Tuendelee…

Clement Mzize mnaesema anazingua, kumbukeni ametoka kuwa top scorer ligi ya under 20, anapandishwa ligi kuu, Coach Nabi anamuamini na kumpa nafasi. Dogo kacheza hadi fainali ya CAF Confederation.. Je alibebwa?

Clement Mzize, baada ya Nabi kuondoka ameendelea kuaminiwa chini ya utawala wa Coach Gamondi

Je Mzize anahonga ili apate namba? Jibu baki nalo.. Chini ya Gamondi, Mzize ndio amekua na msimu bora zaidi.

Mnavyosema Mzize anazingua, Je anazingua sehemu gani? Mkichunguza vizuri Graph ya Mzize tangu anaanza kucheza mpira wa ushindani haijawahi kushuka, kila msimu anapanda.

Je mlitaka Mzize akue kiwango haraka haraka, na kuwa bora kama “Kuku Broiler” ambao wiki tatu mnachinja na kutengeneza “Kuku Roast”?

Je nikisema Mzize ndiye mchezaji kijana wa Kitanzania mwenye thamani kubwa baada ya Feisal Salum mtanikatalia?

Ipo hivi kuna vigezo vya kuitambua thamani halisi ya mcheza soka yeyote. Vigezo hvyo ni;

1 > Umri 2> Kipaji ( Potential ) 3> Uzoefu wa kimataifa 4> Injury Record 5 > Nafasi anayocheza, takwimu zake n.k

Nataka mniambie ni kigezo gani hapo ambacho mzize kinamkataa?

Kati ya strikers vijana tulionao Tanzania, kwenye ligi yetu ni Mzize pekee ambae kwa msimu ulioisha alikua na takwimu bora. Tumuweke pembeni Waziri Junior.

Mzize sio mchezaji ambae anapata sana injury. Lakn pia Mzize umri wake unamruhusu kukua na kuongezeka thamani zaidi

Kuhusu kipaji Mzize anacho kikubwa bila shaka.

Je ni fact ipi hapo inamkataa Mzize? Nani huyo anasemaga Mzize hafai?

Twende kwenye suala la ufundi. Huyu Mzize anacheza nafasi zote za mbele. Winga ya kulia, Kushoto na striker.

Mzize ana mwendo, ana nguvu, anakupa vitu vingi kwenye timu ‘Kimfumo’

Mzize ana technical ability nzuri ya kutumia miguu yote miwili kwa ufasaha. Ana uwezo mzuri wa ku’shoot, kupiga headers zenye unyama mwingi.

Mzize ana mwili wa mapambano, ni aina ya mchezaji ambae ni mpambania chama. Atavuja jasho haswaa kwa ajili ya timu.

Nyie mnadhani wazungu wawili, Nabi na Gamondi kumkubali Mzize ni kazi rahisi?

Mnaomkataa Mzize, mnatumia vigezo gani?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: