Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lingard awindwa Uturuki

Jesse Lingard Nottingham Forest F365 2 Jesse Lingard

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa kati wa Nottingham Forest Jesse Lingard ameonekana kulengwa na vilabu vya Ligi ya Ututuki-Fenerbahce na Besiktas kabla ya dirisha la uhamisho la Uturuki kufungwa wiki hii.

Lingard ndiye aliyesajiliwa na Forest kwa uhamisho wa bure kutoka Manchester United katika harakati zao za kusajili wachezaji majira ya kiangazi. Lakini ameshindwa kutimiza matarajio katika uwanja wa City Ground.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 bado hajapata matokeo anayotaka katika kikosi cha Steve Cooper, kwa kushindwa kufunga au kutoa pasi ya mabao msimu huu kwenye Premier League.

Lingard ameanza mechi 11 pekee kati ya 21 za Ligi Kuu katika timu yake ya Nottingham Forest hadi sasa msimu huu na mabao yake mawili na pasi mbili za mabao amezipata kwenye Kombe la Carabao.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alisaini mkataba wa mwaka mmoja tu na Forest alipowasili majira ya joto.

Lakini Sasa huenda Lingard akajiunga na Fenerbahce au Besiktas kabla ya dirisha la usajili kufungwa siku ya Jumatano.

Fenerbahce na Besiktas wote wanatazamia kuongeza chaguo lao la kiungo kabla ya dirisha la usajili kufungwa na wako tayari kujaribu nia ya kumnasa Lingard.

Fenerbahce kwa sasa wako nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uturuki, pointi sita juu ya Besiktas, walio katika nafasi ya nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live