Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lingard atimkia Korea Kusini

Jesse Lingard Wakala Jesse Lingard

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa zamani wa Manchester United, Jesse Lingard amekamilisha sehemu ya kwanza ya vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na miamba ya Korea Kusini, FC Seoul.

Sehemu ya pili ya vipimo vya afya itafanyika baadae Leo kabla ya kukamilisha uhamisho wake kesho Februari 7, 2024.

Lingard (31) ambaye amewahi kuichezea timu ya Taifa England atafungua ukurasa mpya Mashariki ya mbali huku akitumai kufufua maisha yake ya soka na vigogo hao wa Ligi kuu Korea Kusini.

Lingard almaarufu ‘Lingardinho’ ambaye ni mhitimu wa shule ya vipaji ya Manchester United kwa sasa hana timu baada ya mkataba wake na Nottingham Forest kufikia ukomo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live